Matendo 1:17 - Swahili Revised Union Version kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yuda alikuwa mmoja wa kikundi chetu, maana alichaguliwa ashiriki huduma yetu.” ( Biblia Habari Njema - BHND Yuda alikuwa mmoja wa kikundi chetu, maana alichaguliwa ashiriki huduma yetu.” ( Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yuda alikuwa mmoja wa kikundi chetu, maana alichaguliwa ashiriki huduma yetu.” ( Neno: Bibilia Takatifu Yuda alikuwa mmoja wetu, kwa maana na yeye alichaguliwa ashiriki katika huduma hii.” Neno: Maandiko Matakatifu Yuda alikuwa mmoja wetu, kwa maana na yeye alichaguliwa ashiriki katika huduma hii.” BIBLIA KISWAHILI kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii. |
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.
Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.
Na Barnaba na Sauli, walipokwisha kutimiza huduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemu, wakamchukua pamoja nao Yohana aitwaye Marko.
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake.
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;