Marko 8:32 - Swahili Revised Union Version Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliwaambia jambo hilo waziwazi. Hapo, Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliwaambia jambo hilo waziwazi. Hapo, Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliwaambia jambo hilo waziwazi. Hapo, Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea. Neno: Bibilia Takatifu Aliyasema haya waziwazi. Ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea. Neno: Maandiko Matakatifu Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea. BIBLIA KISWAHILI Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea. |
Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo dada yangu alivyoniacha nifanye kazi peke yangu? Basi mwambie anisaidie.
Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa inakuja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.