Marko 8:26 - Swahili Revised Union Version Akamwagiza aende nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie. Petro Amkiri Yesu kuwa Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru, “Usirudi kijijini!” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru, “Usirudi kijijini!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru, “Usirudi kijijini!” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamtuma nyumbani mwake, akamwambia, “Hata kijijini usiingie.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.” BIBLIA KISWAHILI Akamwagiza aende nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie. |
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila nenda zako, ukajioneshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue.
Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari;
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate katika macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.