Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Marko 7:2 - Swahili Revised Union Version

wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikula mikate kwa mikono najisi, yaani bila kunawa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikula mikate kwa mikono najisi, yaani bila kunawa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikula mikate kwa mikono najisi, yaani bila kunawa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani bila kunawa kama ilivyotakiwa na Torati ya Wayahudi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani, bila kunawa kama ilivyotakiwa na Torati ya dini ya Wayahudi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Marko 7:2
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mbona wanafunzi wako huyavunja mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.


Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi?


Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula.


Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali kwa mtu aliye Myahudi ashirikiane na mtu wa taifa lingine wala kumtembelea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu yeyote mchafu wala najisi.


Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijawahi kuingia kinywani mwangu.


Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?


Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo.