Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,
Marko 2:25 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa akiona njaa na kuhitaji chakula, yeye na wenziwe? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? Neno: Bibilia Takatifu Isa akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi yeye na wenzake walipokuwa na njaa, wakahitaji chakula? Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawajibu, “Je, hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa, wakahitaji chakula? BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa akiona njaa na kuhitaji chakula, yeye na wenziwe? |
Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,
wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umejiandalia sifa?
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni la ajabu machoni petu?
Na kuhusu wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Kuhusu kile kichaka jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?