Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Marko 2:26 - Swahili Revised Union Version

26 Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Yeye aliingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Yeye aliingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Yeye aliingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani tu. Naye pia akawapa wenzake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila mikate ile ya wonesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?

Tazama sura Nakili




Marko 2:26
18 Marejeleo ya Msalaba  

Na tazama, Sadoki naye akaja, na Walawi wote pamoja naye, huku wakilichukua sanduku la Agano la Mungu; kisha wakalitua hilo sanduku la Mungu; Abiathari naye akapanda juu, hadi watu wote walipokwisha kuutoka mji.


Basi Sadoki na Abiathari wakalichukua sanduku la Mungu, wakalirudisha Yerusalemu; wakakaa huko.


Je! Hawako Sadoki na Abiathari, makuhani, pamoja nawe huko? Basi itakuwa, kila neno utakalolisikia katika jumba la mfalme, utawaambia Sadoki na Abiathari, makuhani.


na Shausha mwandishi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani.


na Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;


Akashauriana na Yoabu, mwana wa Seruya, na Abiathari, kuhani; nao wakamsaidia Adonia, wakamfuata.


Mfalme Sulemani akajibu, akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya.


na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa jemadari wa jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani;


Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa koo za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari koo moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.


Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?


Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa akiona njaa na kuhitaji chakula, yeye na wenziwe?


Basi Daudi akaenda Nobu kwa Ahimeleki, kuhani. Ahimeleki akaenda kumlaki Daudi, akitetemeka, akamwambia, Kwa nini uko peke yako, wala hapana mtu pamoja nawe?


Ikawa Abiathari, mwana wa Ahimeleki, alipomkimbilia Daudi huko Keila, alishuka na naivera mkononi mwake.


Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo