akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
Marko 2:1 - Swahili Revised Union Version Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadhaa, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba yupo nyumbani. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani. BIBLIA KISWAHILI Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadhaa, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. |
akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.
Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza kuhusu ule mfano.
Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika.
Alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
Akawaambia, Bila shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.
Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yudea mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa karibu kufa.
Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.