Marko 16:11 - Swahili Revised Union Version Lakini hao waliposikia kwamba yu hai, naye amemwona, hawakuamini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini. Biblia Habari Njema - BHND Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini. Neno: Bibilia Takatifu Lakini waliposikia kwamba Isa yu hai na kwamba Mariamu alikuwa amemwona, hawakusadiki. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini waliposikia kwamba Isa yu hai na kwamba Maria alikuwa amemwona, hawakusadiki. BIBLIA KISWAHILI Lakini hao waliposikia kwamba yu hai, naye amemwona, hawakuamini. |
Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.
Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula chochote hapa?
Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.