Marko 15:3 - Swahili Revised Union Version Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi. Biblia Habari Njema - BHND Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi. Neno: Bibilia Takatifu Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. Neno: Maandiko Matakatifu Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. BIBLIA KISWAHILI Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi. |
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari.