Marko 13:23 - Swahili Revised Union Version Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nyinyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nyinyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nyinyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo jihadharini. Nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo jihadharini. Nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia. BIBLIA KISWAHILI Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. |
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali.
kwa maana watajitokeza Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, ikiwezekana, hata hao wateule.
Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.
Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.
Basi, wapenzi kwa kuwa mmejua hayo, jihadharini msije mkapotoshwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthabiti wenu.