Marko 1:35 - Swahili Revised Union Version Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali. Biblia Habari Njema - BHND Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali. Neno: Bibilia Takatifu Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Isa akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. Neno: Maandiko Matakatifu Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Isa akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. BIBLIA KISWAHILI Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. |
Naye Yesu aliposikia hayo, aliondoka huko katika mashua, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao.
Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenituma, nikaimalize kazi yake.
Kisha Yesu, alipotambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;