Akasema, Hasha, BWANA, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
Maombolezo 5:9 - Swahili Revised Union Version Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu, maana wauaji wanazurura huko mashambani. Biblia Habari Njema - BHND Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu, maana wauaji wanazurura huko mashambani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu, maana wauaji wanazurura huko mashambani. Neno: Bibilia Takatifu Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani. Neno: Maandiko Matakatifu Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani. BIBLIA KISWAHILI Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani. |
Akasema, Hasha, BWANA, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
kwa sababu ya Wakaldayo; maana waliwaogopa, kwa sababu Ishmaeli, mwana wa Nethania, amemwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala juu ya nchi.
mkisema, La! Lakini tutakwenda nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita, wala kuisikia sauti ya tarumbeta, wala kuona njaa kwa kukosa chakula; nasi tutakaa huko;
basi, itakuwa, upanga mnaouogopa utawapata huko, katika nchi ya Misri, nayo njaa mnayoiogopa itawafuatia mbio huko Misri, nanyi mtakufa huko.
Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwaabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.