Maombolezo 5:20 - Swahili Revised Union Version Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mbona umetuacha muda mrefu hivyo? Mbona umetutupa siku nyingi hivyo? Biblia Habari Njema - BHND Mbona umetuacha muda mrefu hivyo? Mbona umetutupa siku nyingi hivyo? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mbona umetuacha muda mrefu hivyo? Mbona umetutupa siku nyingi hivyo? Neno: Bibilia Takatifu Kwa nini watusahau siku zote? Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu? Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nini watusahau siku zote? Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu? BIBLIA KISWAHILI Mbona watusahau siku zote; Na kutuacha muda huu mwingi? |
Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?
Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;
Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.