Maombolezo 3:26 - Swahili Revised Union Version Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa bwana. BIBLIA KISWAHILI Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu. |
Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yuko pamoja nanyi.
Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.
Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.
Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.
Kwa maana msaada wa Misri haufai kitu na ni bure; Kwa hiyo nimemwita, “Rahabu aketiye kimya”.
ukamwambie, Hadhari, tulia; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia.
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu.
Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
Kwa hiyo iweni tayari, na makini; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.