Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 3:26 - Swahili Revised Union Version

26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Ni vema mtu kungojea kwa saburi ukombozi utokao kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 3:26
24 Marejeleo ya Msalaba  

Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.


Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yuko pamoja nanyi.


Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako, Na maagizo yako nimeyatenda.


Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, Na sheria yako ndiyo furaha yangu.


Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia.


Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.


Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.


Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.


Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.


Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.


Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.


Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako sifa, Ee Uliye Juu.


Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.


BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.


Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.


Kwa maana msaada wa Misri haufai kitu na ni bure; Kwa hiyo nimemwita, “Rahabu aketiye kimya”.


ukamwambie, Hadhari, tulia; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia.


Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.


Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.


Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.


Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu.


Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;


Kwa hiyo iweni tayari, na makini; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo