Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Maombolezo 3:19 - Swahili Revised Union Version

Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu kwanipa uchungu kama wa nyongo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu kwanipa uchungu kama wa nyongo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu kwanipa uchungu kama wa nyongo.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Maombolezo 3:19
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa, Ee Mungu, mkuu, mwenye uweza, Mungu wa kuogofya, mwenye kushika maagano na rehema, mashaka yote yaliyotupata sisi, wafalme wetu, na wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote, tangu zamani za wafalme wa Ashuru hata leo, na yasihesabiwe kuwa ni madogo.


Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.


BWANA, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika.


Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu; Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!


Ukumbuke, Ee Bwana, Wanavyosimangwa watumishi wako; Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu Masimango ya watu wengi.


Mbona tunakaa kimya? Jikusanyeni, tukaingie ndani ya miji yenye maboma, tukanyamaze humo kwa maana BWANA, Mungu wetu, ametunyamazisha, naye ametupa maji yenye uchungu tunywe, kwa sababu tumemwasi BWANA.


Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji yenye sumu wayanywe.


Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga.


Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu.