Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
Maombolezo 1:11 - Swahili Revised Union Version Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa Yerusalemu wote wanahangaika kutafuta chakula; hazina zao wanazitoa kupata chakula, wajirudishie nguvu zao. Nao mji unalia, “Hebu niangalie, ee Mwenyezi-Mungu, ona jinsi nilivyogeuka kuwa duni. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa Yerusalemu wote wanahangaika kutafuta chakula; hazina zao wanazitoa kupata chakula, wajirudishie nguvu zao. Nao mji unalia, “Hebu niangalie, ee Mwenyezi-Mungu, ona jinsi nilivyogeuka kuwa duni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa Yerusalemu wote wanahangaika kutafuta chakula; hazina zao wanazitoa kupata chakula, wajirudishie nguvu zao. Nao mji unalia, “Hebu niangalie, ee Mwenyezi-Mungu, ona jinsi nilivyogeuka kuwa duni. Neno: Bibilia Takatifu Watu wake wote wanalia kwa uchungu watafutapo chakula; wanabadilisha hazina zao kwa chakula ili waweze kuendelea kuishi. “Tazama, Ee Mwenyezi Mungu, uangalie; kwa maana nimedharauliwa.” Neno: Maandiko Matakatifu Watu wake wote wanalia kwa uchungu watafutapo chakula; wanabadilisha hazina zao kwa chakula ili waweze kuendelea kuishi. “Tazama, Ee bwana, ufikiri, kwa maana nimedharauliwa.” BIBLIA KISWAHILI Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge. |
Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejesha, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.
Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.
Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hakuna mkate kabisa katika mji.
Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwezi, njaa ilizidi sana ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.
Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.
Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.
Wao huwauliza mama zao, Ziko wapi nafaka na divai? Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwa Katika mitaa ya mji, Hapo walipomiminika nafsi zao Vifuani mwa mama zao.
Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?