Na mji wowote au kijiji chochote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hadi mtakapotoka.
Luka 9:4 - Swahili Revised Union Version Na nyumba yoyote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyumba yoyote mtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humo mpaka mtakapoondoka katika kijiji hicho. Biblia Habari Njema - BHND Nyumba yoyote mtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humo mpaka mtakapoondoka katika kijiji hicho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyumba yoyote mtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humo mpaka mtakapoondoka katika kijiji hicho. Neno: Bibilia Takatifu Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. Neno: Maandiko Matakatifu Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. BIBLIA KISWAHILI Na nyumba yoyote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini. |
Na mji wowote au kijiji chochote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hadi mtakapotoka.
Akawaambia, Mahali popote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hadi mtakapotoka mahali pale.
Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili.
Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung'uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.