Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Luka 8:9 - Swahili Revised Union Version Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanafunzi wake Yesu wakamwuliza maana ya mfano huo. Biblia Habari Njema - BHND Wanafunzi wake Yesu wakamwuliza maana ya mfano huo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanafunzi wake Yesu wakamwuliza maana ya mfano huo. Neno: Bibilia Takatifu Wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo. Neno: Maandiko Matakatifu Wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo. BIBLIA KISWAHILI Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo? |
Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia katika nyumba; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.
Naye alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Kumi na Wawili, walimwuliza kuhusu ile mifano.
wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.
Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.