Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, majusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Luka 7:17 - Swahili Revised Union Version Habari hii yake ikaenea kote katika Yudea yote, na katika nchi zote za karibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Habari hizo zikaenea kote katika Yudea na katika nchi za jirani. Biblia Habari Njema - BHND Habari hizo zikaenea kote katika Yudea na katika nchi za jirani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Habari hizo zikaenea kote katika Yudea na katika nchi za jirani. Neno: Bibilia Takatifu Habari hizi za mambo aliyoyafanya Isa zikaenea Yudea yote na sehemu zote za jirani. Neno: Maandiko Matakatifu Habari hizi za mambo aliyoyafanya Isa zikaenea Uyahudi wote na sehemu zote za jirani. BIBLIA KISWAHILI Habari hii yake ikaenea kote katika Yudea yote, na katika nchi zote za karibu. |
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, majusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Naye Mfalme Herode akasikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa limeenea, akasema, Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake.
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaendea Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.