Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Luka 4:4 - Swahili Revised Union Version Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’ ” BIBLIA KISWAHILI Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. |
Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi.
Waache watoto wako wasio na baba, mimi nitawahifadhi hai, na wajane wako na wanitumaini mimi.
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Akakunyenyekeza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA.