Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Luka 24:11 - Swahili Revised Union Version hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini. Biblia Habari Njema - BHND Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini. Neno: Bibilia Takatifu Lakini hawakuwasadiki hao wanawake, kwa sababu maneno yao yalionekana kama upuzi. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini hawakuwasadiki hao wanawake, kwa sababu maneno yao yalionekana kama upuzi. BIBLIA KISWAHILI hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo. |
Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Basi yule afisa, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.
Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula chochote hapa?
Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.