Luka 23:9 - Swahili Revised Union Version Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lolote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu hakumjibu neno. Biblia Habari Njema - BHND Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu hakumjibu neno. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu hakumjibu neno. Neno: Bibilia Takatifu Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Isa hakumjibu lolote. Neno: Maandiko Matakatifu Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Isa hakumjibu lolote. BIBLIA KISWAHILI Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lolote. |
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.
Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetoka wapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lolote.
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.