Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Luka 21:18 - Swahili Revised Union Version Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea. Biblia Habari Njema - BHND Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea. Neno: Bibilia Takatifu Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. BIBLIA KISWAHILI Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. |
Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko Shomoro wengi.
Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea.
Lakini watu wakamwambia Sauli, Je! Atakufa Yonathani, ambaye ndiye aliyeufanya huo wokovu mkuu katika Israeli? Hasha! Kama aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa kichwa chake; kwa maana ametenda kazi pamoja na Mungu leo. Hivyo hao watu wakamponya Yonathani, asife.
Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya kombeo.