akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.
Luka 18:37 - Swahili Revised Union Version Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.” Biblia Habari Njema - BHND Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.” Neno: Bibilia Takatifu Wakamwambia, “Isa Al-Nasiri anapita.” Neno: Maandiko Matakatifu Wakamwambia, “Isa Al-Nasiri anapita.” BIBLIA KISWAHILI Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita. |
akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.
Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.
Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.
Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.
Enyi wanaume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;
jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama akiwa mzima mbele yenu.
(Kwa maana asema, Kwa wakati uliokubalika nilikusikia, Na katika siku ya wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)