Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 2:23 - Swahili Revised Union Version

23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 akaenda kuishi katika mji ulioitwa Nasiri. Hivyo likawa limetimia neno lililonenwa na manabii waliposema, “Ataitwa Mnasiri.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 akaenda akaishi katika mji ulioitwa Nasiri. Hivyo likawa limetimia neno lililonenwa na manabii, “Ataitwa Mnasiri.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.

Tazama sura Nakili




Mathayo 2:23
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania;


Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,


Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.


Naye alipotoka nje hadi ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti.


akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?


Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.


Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka katika mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,


Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.


Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.


Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.


Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.


Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.


Enyi wanaume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Kwa maana tumemwona mtu huyu kuwa mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazareti.


kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.


Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo