Luka 12:31 - Swahili Revised Union Version Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu, na hayo mtapewa kwa ziada. Biblia Habari Njema - BHND Shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu, na hayo mtapewa kwa ziada. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu, na hayo mtapewa kwa ziada. Neno: Bibilia Takatifu Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia. Neno: Maandiko Matakatifu Bali utafuteni Ufalme wa Mwenyezi Mungu, na haya yote atawapa pia. BIBLIA KISWAHILI Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa. |
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang'anywa.
kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.