Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Luka 1:7 - Swahili Revised Union Version Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. Biblia Habari Njema - BHND Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. Neno: Bibilia Takatifu Lakini walikuwa hawana watoto, kwa sababu Elizabeti alikuwa tasa; nao wote wawili walikuwa wazee sana. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini walikuwa hawana watoto, kwa sababu Elizabeti alikuwa tasa; nao wote wawili walikuwa wazee sana. BIBLIA KISWAHILI Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. |
Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Basi Abrahamu na Sara walikuwa wazee wenye umri mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea dada yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
Mfalme Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate joto.
Zamani za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.
Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia moja), na hali ya utasa wa tumbo lake Sara.
Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto.