Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
Isaya 7:15 - Swahili Revised Union Version Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atakula siagi na asali mpaka atakapojua kukataa mabaya na kuchagua mema. Biblia Habari Njema - BHND Atakula siagi na asali mpaka atakapojua kukataa mabaya na kuchagua mema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atakula siagi na asali mpaka atakapojua kukataa mabaya na kuchagua mema. Neno: Bibilia Takatifu Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. Neno: Maandiko Matakatifu Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. BIBLIA KISWAHILI Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema. |
Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
kisha itakuwa, kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi, atakula siagi; kwa maana kila mtu aliyesalia katika nchi hii atakula siagi na asali.
Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.
Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu zake Aliye Juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Tena, wadogo wenu, mliosema watakuwa mateka, na wana wenu, wasiokuwa leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki.