Isaya 61:9 - Swahili Revised Union Version Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika makabila ya watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa; watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine. Kila atakayewaona atakiri kwamba wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa; watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine. Kila atakayewaona atakiri kwamba wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa; watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine. Kila atakayewaona atakiri kwamba wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, na uzao wao miongoni mwa makabila ya watu. Wale wote watakaowaona watatambua kuwa ni taifa ambalo Mwenyezi Mungu amelibariki.” Neno: Maandiko Matakatifu Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, na uzao wao miongoni mwa kabila za watu. Wale wote watakaowaona watatambua kuwa ni taifa ambalo bwana amelibariki.” BIBLIA KISWAHILI Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika makabila ya watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA. |
Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba BWANA amenibariki kwa ajili yako.
Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;
Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;
Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.
Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.
Maana BWANA asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee BWANA, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli.
Kisha itakuwa, kama vile mlivyokuwa laana katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na nyumba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini mikono yenu na iwe hodari.
Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.
Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.