Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 61:8 - Swahili Revised Union Version

8 Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyanganyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyanganyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyang'anyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 “Kwa maana Mimi, Mwenyezi Mungu, napenda haki, na ninachukia unyang’anyi na uovu. Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao na kufanya agano la milele nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 “Kwa maana Mimi, bwana, napenda haki, na ninachukia unyang’anyi na uovu. Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao na kufanya agano la milele nao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.

Tazama sura Nakili




Isaya 61:8
34 Marejeleo ya Msalaba  

Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.


Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.


Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele.


Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.


Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.


Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za BWANA.


Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.


Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.


Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.


Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.


Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.


Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu.


Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.


Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.


bali BWANA wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki.


Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.


Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.


BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.


Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.


nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache.


bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,


Walakini nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe, katika siku za ujana wako, nami nitaweka imara agano la milele pamoja nawe.


Nami nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni.


Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA.


Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.


Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na subira ya Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo