Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Isaya 48:14 - Swahili Revised Union Version

Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Kusanyikeni nyote msikilize! Nani kati ya miungu yenu aliyetabiri vitu hivi? Mimi Mwenyezi-Mungu nampenda Koreshi; yeye atatekeleza lengo langu kuhusu Babuloni, naam, yeye atawashambulia Wakaldayo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Kusanyikeni nyote msikilize! Nani kati ya miungu yenu aliyetabiri vitu hivi? Mimi Mwenyezi-Mungu nampenda Koreshi; yeye atatekeleza lengo langu kuhusu Babuloni, naam, yeye atawashambulia Wakaldayo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Kusanyikeni nyote msikilize! Nani kati ya miungu yenu aliyetabiri vitu hivi? Mimi Mwenyezi-Mungu nampenda Koreshi; yeye atatekeleza lengo langu kuhusu Babuloni, naam, yeye atawashambulia Wakaldayo.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize: Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu ambayo imetabiri vitu hivi? Watu wa Mwenyezi Mungu waliochaguliwa na kuungana watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli; mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize: Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu ambayo imetabiri vitu hivi? Watu wa bwana waliochaguliwa na kuungana watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli; mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Isaya 48:14
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku zijazo.

Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.

Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.

Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.

Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuoneshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye.

Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.

nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.

Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze.

Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.

Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?

Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Nenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.