Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 43:9 - Swahili Revised Union Version

9 Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mataifa yote na yakusanyike, watu wote na wakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia? Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa? Wawalete mashahidi wao kuthibitisha kwamba walifanya hivyo. Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mataifa yote na yakusanyike, watu wote na wakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia? Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa? Wawalete mashahidi wao kuthibitisha kwamba walifanya hivyo. Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mataifa yote yanakutanika pamoja, na makabila yanakusanyika. Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya, na kututangazia mambo yaliyopita? Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi, ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

BIBLIA KISWAHILI

9 Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.

Tazama sura Nakili

Isaya 43:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hadi machweo yake.

Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.

Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu.

Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.

nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.

Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.

Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; niliyatenda kwa ghafla, yakatokea.

Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko wateremshe mashujaa wako wote, Ee BWANA.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo