Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
Isaya 43:8 - Swahili Revised Union Version Walete watu wasioona, japo wana macho, wasiosikia japo wana masikio. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waleteni mbele watu hao, ambao wana macho lakini hawaoni wana masikio lakini hawasikii! Biblia Habari Njema - BHND Waleteni mbele watu hao, ambao wana macho lakini hawaoni wana masikio lakini hawasikii! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waleteni mbele watu hao, ambao wana macho lakini hawaoni wana masikio lakini hawasikii! Neno: Bibilia Takatifu Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni, wenye masikio lakini hawasikii. Neno: Maandiko Matakatifu Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni, wenye masikio lakini hawasikii. BIBLIA KISWAHILI Walete watu wasioona, japo wana macho, wasiosikia japo wana masikio. |
Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.
Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamuoni; mlio na masikio ila hamsikii.
Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.
ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.