Isaya 38:16 - Swahili Revised Union Version Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda, kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi. Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi. Biblia Habari Njema - BHND “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda, kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi. Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda, kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi. Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi. Neno: Bibilia Takatifu Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi, nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia. Uliniponya na kuniacha niishi. Neno: Maandiko Matakatifu Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi, nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia. Uliniponya na kuniacha niishi. BIBLIA KISWAHILI Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha. |
Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.
Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.
Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
Akakunyenyekeza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA.
Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?