Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 38:15 - Swahili Revised Union Version

15 Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini niseme nini: Yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini niseme nini: Yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini niseme nini: yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Lakini niseme nini? Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili. Nitatembea kwa unyenyekevu katika miaka yangu yote kwa sababu ya haya maumivu makali ya nafsi yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Lakini niseme nini? Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili. Nitatembea kwa unyenyekevu katika miaka yangu yote kwa sababu ya haya maumivu makali ya nafsi yangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.

Tazama sura Nakili

Isaya 38:15
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.

Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.

Na sasa, Ee Mungu wetu, tuseme nini baada ya hayo? Maana tumeziacha amri zako,

Nayachukia maisha yangu; Nitayasema malalamiko yangu wazi; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.

Mwingine hufa katika uchungu wa roho, Asionje mema kamwe.

Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.

Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.

Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.

Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.

Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao?

Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo