Isaya 32:5 - Swahili Revised Union Version Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mlaghai hataitwa kuwa ni mheshimiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wapumbavu hawataitwa tena waungwana, wala walaghai hawataitwa tena waheshimiwa. Biblia Habari Njema - BHND Wapumbavu hawataitwa tena waungwana, wala walaghai hawataitwa tena waheshimiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wapumbavu hawataitwa tena waungwana, wala walaghai hawataitwa tena waheshimiwa. Neno: Bibilia Takatifu Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu. Neno: Maandiko Matakatifu Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu. BIBLIA KISWAHILI Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mlaghai hataitwa kuwa ni mheshimiwa. |
Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.
Tena vyombo vyake mlaghai ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki.
Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.
Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.