Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 32:6 - Swahili Revised Union Version

6 Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa bila chakula, na kuwanyima kinywaji wenye kiu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu Mwenyezi Mungu; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, na wenye kiu huwanyima maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu bwana; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, na wenye kiu huwanyima maji.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa bila chakula, na kuwanyima kinywaji wenye kiu.

Tazama sura Nakili




Isaya 32:6
33 Marejeleo ya Msalaba  

Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.


Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA.


Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni.


ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang'anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!


Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.


Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa BWANA.


Ni nini maana yake, ninyi kuwaonea watu wangu, na kuponda nyuso za maskini? Asema Bwana, BWANA wa majeshi.


Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu.


katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.


Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia zao kuu.


Kwa sababu hiyo Bwana hatawafurahia vijana wao, wala hatawahurumia yatima zao wala wajane wao; maana kila mtu ni mnajisi, dhalimu, na kila ulimi hunena upumbavu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoadoa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.


Je! Mwaona ya kuwa ni neno dogo ninyi kulishwa malisho mema, hata mkawa hamna budi kukanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia? Na kuwa mmekunywa maji yaliyo safi, nanyi hamna budi kuyatibua kwa miguu yaliyobaki?


Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.


tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu; na kuziuza takataka za ngano.


Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;


Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.


Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.


Kama vile walivyosema watu wa kale katika mithali yao, Katika waovu hutoka uovu; ila mkono wangu hautakuwa juu yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo