Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.
Isaya 3:2 - Swahili Revised Union Version mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ataondoa mashujaa na askari, waamuzi na manabii, waaguzi na wazee, Biblia Habari Njema - BHND Ataondoa mashujaa na askari, waamuzi na manabii, waaguzi na wazee, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ataondoa mashujaa na askari, waamuzi na manabii, waaguzi na wazee, Neno: Bibilia Takatifu shujaa na mtu wa vita, mwamuzi na nabii, mwaguzi na mzee, Neno: Maandiko Matakatifu shujaa na mtu wa vita, mwamuzi na nabii, mwaguzi na mzee, BIBLIA KISWAHILI mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; |
Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.
jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye stadi, na mganga ajuaye uganga sana.
Waambie sasa nyumba hii iliyoasi, Hamjui maana ya mambo haya? Waambie, Tazama, mfalme wa Babeli alifika Yerusalemu, akamtwaa mfalme wake, na wakuu wake, akawachukua pamoja naye mpaka Babeli;
akawatwaa baadhi ya wazao wa kifalme; kisha akafanya agano naye, akamwapisha; akawaondoa watu wa nchi wenye nguvu;
Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.
Na hao wengine aliwaambia, nami nilisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma;
nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA.