Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 3:1 - Swahili Revised Union Version

1 Kwa maana, tazama, Bwana, BWANA wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Sasa, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataondoa kutoka Yerusalemu na Yuda kila tegemeo: Tegemeo lote la chakula, na tegemeo lote la kinywaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Sasa, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataondoa kutoka Yerusalemu na Yuda kila tegemeo: Tegemeo lote la chakula, na tegemeo lote la kinywaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Sasa, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataondoa kutoka Yerusalemu na Yuda kila tegemeo: tegemeo lote la chakula, na tegemeo lote la kinywaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Tazama sasa, Bwana, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda upatikanaji wa mahitaji na misaada, upatikanaji wote wa chakula na tegemeo lote la maji,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Tazama sasa, Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda upatikanaji wa mahitaji na misaada, upatikanaji wote wa chakula na tegemeo lote la maji,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Kwa maana, tazama, Bwana, BWANA wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji;

Tazama sura Nakili




Isaya 3:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.


Akasababisha njaa katika nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.


Kwa hiyo, asema Bwana, BWANA wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitalipiza kisasi kwa adui zangu;


Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake iko katika mianzi ya pua yake; kwa maana wanafaa kitu gani?


BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;


Lakini yule kamanda akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma niseme, maneno haya kwa bwana wako na kwako wewe? Hakunituma pia kwa watu hawa wanaokaa ukutani, wanaokabiliwa na tisho la kula mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?


Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


Hupokonya upande wa mkono wa kulia, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.


Ndipo Sedekia mfalme akatoa amri, wakamtia Yeremia katika ukumbi wa walinzi; wakampa kila siku mkate mmoja uliotoka katika njia ya waokaji, hata mkate wote wa mji ulipokwisha. Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.


Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hakuna mkate kabisa katika mji.


Maana, kwa sababu ya hasira ya BWANA, mambo haya yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata akawaondosha wasiwe mbele za uso wake, naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.


Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwezi, njaa ilizidi sana ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.


Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa.


Mwanadamu, nchi itakapofanya dhambi na kuniasi, kwa kukosa, nikaunyosha mkono wangu juu yake, na kulivunja tegemeo la chakula chake, na kuiletea njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama;


Hapo nitakapovunja tegemeo lenu la mkate, wanawake kumi wataoka mikate yenu katika tanuri moja, nao watawapa mikate yenu tena kwa kupima kwa mizani; nanyi mtakula, lakini hamtashiba.


Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.


Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako, mshauri wako amepotea, hata umeshikwa na uchungu kama mwanamke wakati wa kuzaa?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo