Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
Isaya 2:10 - Swahili Revised Union Version Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele za utukufu wa enzi yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ingieni katika mwamba, mkajifiche mavumbini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake. Biblia Habari Njema - BHND Ingieni katika mwamba, mkajifiche mavumbini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ingieni katika mwamba, mkajifiche mavumbini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake. Neno: Bibilia Takatifu Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa enzi yake! Neno: Maandiko Matakatifu Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa bwana na utukufu wa enzi yake! BIBLIA KISWAHILI Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele za utukufu wa enzi yake. |
Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake.
Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa yako wewe; kwa kuwa miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika hali yao ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama wewe.
BWANA asema hivi, Jinsi iyo hiyo nitakiharibu kiburi cha Yuda, na kiburi kikuu cha Yerusalemu.
Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanamu; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.
watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;