Hosea 8:3 - Swahili Revised Union Version Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Israeli amepuuza mambo mema, kwa hiyo, sasa adui watamfuatia. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Israeli amepuuza mambo mema, kwa hiyo, sasa adui watamfuatia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Israeli amepuuza mambo mema, kwa hiyo, sasa adui watamfuatia. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Israeli amekataa lile lililo jema, adui atamfuatia. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Israeli amekataa lile lililo jema, adui atamfuatia. BIBLIA KISWAHILI Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia. |
Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani.
Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nilikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.
Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararuararua daima, akaishika ghadhabu yake milele;
BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huku na huko katika falme zote za duniani.