Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Amosi 1:11 - Swahili Revised Union Version

11 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararuararua daima, akaishika ghadhabu yake milele;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Waliwawinda ndugu zao Waisraeli kwa mapanga, wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu. Hasira yao haikuwa na kikomo, waliiacha iwake daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Waliwawinda ndugu zao Waisraeli kwa mapanga, wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu. Hasira yao haikuwa na kikomo, waliiacha iwake daima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, alikataa kuonesha huruma yoyote, kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Hili ndilo bwana asemalo: “Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, alikataa kuonyesha huruma yoyote, kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararuararua daima, akaishika ghadhabu yake milele;

Tazama sura Nakili

Amosi 1:11
28 Marejeleo ya Msalaba  

Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;

tazama, jinsi wanavyotulipa, wakija kututupa toka milki yako, uliyoturithisha.

Kwa kuwa Waedomi walikuwa wamekuja tena, na kuwapiga Yuda, na kuwachukua wafungwa.

Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!

Je! Utatufanyia hasira hata milele? Utadumisha ghadhabu kizazi hadi kizazi?

Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya.

Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia.

Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.

Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hadumishi hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.

Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.

Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo;

Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwapondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele.

Hivyo mwigeni Mungu, kama watoto wanaopendwa;

Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo