Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.
Hosea 8:12 - Swahili Revised Union Version Nijapomwandikia sheria yangu katika amri makumi elfu, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi, wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu. Biblia Habari Njema - BHND Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi, wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi, wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu. Neno: Bibilia Takatifu Niliwaandikia mambo mengi yaliyohusu sheria yangu, lakini waliziangalia kama kitu kigeni. Neno: Maandiko Matakatifu Nimeandika kwa ajili yao mambo mengi kuhusu sheria yangu, lakini wameziangalia kama kitu cha kigeni. BIBLIA KISWAHILI Nijapomwandikia sheria yangu katika amri makumi elfu, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni. |
Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.
Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA;
Nikawapa amri zangu, na kuwaonesha hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.