Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, licha ya wingi wa watu wake; na watakaobaki watakuwa wachache sana na dhaifu.
Hosea 10:15 - Swahili Revised Union Version Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli, kwa sababu ya uovu wenu mkuu. Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza. Biblia Habari Njema - BHND Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli, kwa sababu ya uovu wenu mkuu. Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli, kwa sababu ya uovu wenu mkuu. Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza. Neno: Bibilia Takatifu Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli, kwa sababu uovu wako ni mkuu. Siku ile itakapopambazuka, mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa. Neno: Maandiko Matakatifu Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli, kwa sababu uovu wako ni mkuu. Siku ile itakapopambazuka, mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa. BIBLIA KISWAHILI Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa. |
Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, licha ya wingi wa watu wake; na watakaobaki watakuwa wachache sana na dhaifu.
Kwa sababu hiyo fitina itatokea kati ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa, kama vile Shalmani alivyoharibu Betharbeli, katika siku ya vita; mama akavunjikavunjika pamoja na watoto wake.
Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi BWANA; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini?
Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.
Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? La hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.