Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 10:14 - Swahili Revised Union Version

14 Kwa sababu hiyo fitina itatokea kati ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa, kama vile Shalmani alivyoharibu Betharbeli, katika siku ya vita; mama akavunjikavunjika pamoja na watoto wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako; ngome zako zote zitaharibiwa, kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani, kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako; ngome zako zote zitaharibiwa, kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani, kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako; ngome zako zote zitaharibiwa, kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani, kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa: kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita, wakati mama pamoja na watoto wao walipotupwa kwa nguvu ardhini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako, ili kwamba ngome zako zote zitaharibiwa: kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita, wakati mama pamoja na watoto wao walipotupwa kwa nguvu ardhini.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Kwa sababu hiyo fitina itatokea kati ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa, kama vile Shalmani alivyoharibu Betharbeli, katika siku ya vita; mama akavunjikavunjika pamoja na watoto wake.

Tazama sura Nakili




Hosea 10:14
21 Marejeleo ya Msalaba  

Uniokoe sasa kutoka kwa mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi ninamwogopa, asije akaniua, na kina mama pamoja na watoto.


Wakaziacha amri zote za BWANA, Mungu wao, wajitengenezea sanamu za kusubu, yaani, ndama wawili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.


Naye Shalmanesa mfalme wa Ashuru akakwea juu yake, Hoshea akawa mtumishi wake, akampa kodi.


Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake wakati wowote na mkono wa mfalme wa Ashuru?


Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.


Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?


Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.


Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa.


Samaria atachukua hatia yake; kwa maana amemwasi Mungu wake; wataanguka kwa upanga; watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande, na wanawake wao wenye mimba watatumbuliwa.


Kwani katika siku ile nitakapompatiliza Israeli makosa yake, nitazipatiliza pia madhabahu za Betheli, na pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali, na kuanguka chini.


Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?


Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Nili, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.


nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha;


Hata hivyo alichukuliwa mbali, alikwenda utumwani; watoto wake wachanga walisetwa kwenye maachano ya njia kuu zote; watu wake wenye heshima wakapigiwa kura, na wakuu wake wote wakafungwa kwa minyororo.


Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye.


Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana huirundikia udongo, na kuitwaa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo