Naye mfalme akawaamuru watu wote, akasema, Mfanyieni BWANA, Mungu wenu, Pasaka, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha agano.
Hesabu 9:2 - Swahili Revised Union Version Tena, wana wa Israeli na waadhimishe sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Waisraeli sharti waiadhimishe sikukuu ya Pasaka wakati uliopangwa. Biblia Habari Njema - BHND “Waisraeli sharti waiadhimishe sikukuu ya Pasaka wakati uliopangwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Waisraeli sharti waiadhimishe sikukuu ya Pasaka wakati uliopangwa. Neno: Bibilia Takatifu “Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. Neno: Maandiko Matakatifu “Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. BIBLIA KISWAHILI Tena, wana wa Israeli na waadhimishe sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. |
Naye mfalme akawaamuru watu wote, akasema, Mfanyieni BWANA, Mungu wenu, Pasaka, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha agano.
Naye Yosia akamfanyia BWANA Pasaka huko Yerusalemu; wakachinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
Kisha, wana wa uhamisho wakaifanya Pasaka, mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi.
Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaiadhimisha kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoisherehekea.
Katika siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile Pasaka?
Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko.