Watoto wao nao uliwaongeza kama nyota za mbinguni, ukawaingiza katika nchi ile, uliyowaambia baba zao kuwa wataingia kuimiliki.
Hesabu 26:51 - Swahili Revised Union Version Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730). Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730. Biblia Habari Njema - BHND Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730. Neno: Bibilia Takatifu Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa elfu mia sita na moja mia saba na thelathini (601,730). Neno: Maandiko Matakatifu Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730. BIBLIA KISWAHILI Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730). |
Watoto wao nao uliwaongeza kama nyota za mbinguni, ukawaingiza katika nchi ile, uliyowaambia baba zao kuwa wataingia kuimiliki.
Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu elfu mia sita wanaume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto.
kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya wanaume elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550).
hao wote waliohesabiwa walikuwa ni wanaume elfu mia sita na tatu, mia tano na hamsini (603,550).
Musa akasema, Watu hawa ambao mimi ni kati yao, ni watu elfu mia sita waendao kwa miguu; nawe umesema, Nitawapa nyama, ili wale muda wa mwezi mzima.
Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa nyumba za baba zao; wote waliohesabiwa katika kambi kwa majeshi yao, walikuwa elfu mia sita na tatu na mia tano na hamsini.