Hesabu 26:42 - Swahili Revised Union Version Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu; Biblia Habari Njema - BHND Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu; Neno: Bibilia Takatifu Hawa walikuwa wazao wa Dani kwa koo zao: kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizo zilikuwa koo za Dani: Neno: Maandiko Matakatifu Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao: kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani: BIBLIA KISWAHILI Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. |
Katika wana wa Dani, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia sita.
Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne.