Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu na Yeriko.
Hesabu 26:3 - Swahili Revised Union Version Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia, Biblia Habari Njema - BHND Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya mto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia, Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Musa na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ng’ambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Musa na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ng’ambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, BIBLIA KISWAHILI Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, |
Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu na Yeriko.
Fanyeni hesabu ya watu, kuanzia umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri.
Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo kambini katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapiga kambi katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko.
Kisha BWANA akanena na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko, akamwambia,
Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. BWANA akamwonesha nchi yote ya Gileadi hata Dani;
Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.
Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha.